1. HUDUMA
Event Yetu itatoa huduma za kadi za mwaliko za kidigitali, ujumbe mfupi wa SMS za taarifa na ukumbusho, pamoja na ubunifu wa event kulingana na makubaliano yaliyofikiwa na mteja.
2. MASHARTI YA MALIPO
Malipo ya awali ya asilimia 100% yatatolewa ili kuthibitisha booking ya huduma. Kushindwa kukamilisha malipo kunaweza kusababisha kutopokea huduma bila taarifa zaidi.
3. HUDUMA ZA ZIADA
Huduma yoyote ya ziada itakayohitajika nje ya kifurushi kilichochaguliwa italazimika kulipiwa mapema kabla ya utekelezaji wake.
4. UTHIBITISHO WA BOOKING
Booking itahesabika kuwa imethibitishwa rasmi baada ya kupokea malipo ya awali ya asilimia 60%.
5. MAKUBALIANO
Kwa kufanya malipo, mteja anakubaliana na masharti na vigezo vyote vilivyobainishwa katika mkataba huu.
6. SERA YA KUGHARIMIA KUGHAIRISHA (CANCELLATION POLICY)
Endapo mteja ataamua kughairi huduma baada ya kuthibitisha booking, masharti yafuatayo yatatumika:
- Malipo ya awali ya asilimia 60% hayatakuwa ya kurejeshwa (non-refundable).
- Endapo kughairi kutafanyika chini ya siku 3 kabla ya tarehe ya tukio, mteja atalazimika kulipa gharama zote zilizokwisha tumika au kuandaliwa kwa ajili ya tukio.
- Event Yetu haitawajibika kwa hasara yoyote itakayotokana na kughairi kwa mteja.